SOMO KUHUSU KUZIMU
SOMO KUHUSU KUZIMU
*SEHEMU YA TATU*
Kwa nini inaitwa mauti ya pili? Ni kwa sababu japo tajiri yuko kwenye mateso na hayuko duniani tena (yaani alishakufa); japo wale malaika walio kifungoni wako kwenye mateso sasa; lakini iko mauti nyingine tofauti nay a sasa. Kitendo cha kutupwa kwenye ziwa la moto (jehanamu) na kubaki humo milele ndicho kinachoitwa mauti ya pili.
✍Hata roho hii ya mauti inayotutoa duniani sasa pamoja na kuzimu aliko shetani sasa navyo vitaingia jehanamu kwenye mauti ya pili:
Imeandikwa: *Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. (Ufu 20:14)*
*JE, ROHO ZILIZOONDOKA DUNIANI ZINAKUWA KATIKA HALI GANI?*
Hawa ni watu kamili kama tulivyo sisi. Sisi kama roho tumo ndani ya mwili wa nyama, lakini ukivua mwili huu (yaani, ukifa) unavikwa mwili wa kiroho; na unaendelea kuishi kama kawaida.
Biblia inasema: *Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. (1Kor 15:40)*
✍Tofauti ni majukumu tu. Huku tunafanya kazi, tunasafiri, n.k. Lakini kule wenye dhambi wanateswa na watakatifu wanamfurahia Yesu, kwa mfano kwa kusifu.
*HITIMISHO*
Kuzimu ni mahali aliko shetani sasa hivi pamoja na wanadamu wote wanaokufa katika dhambi. Haya ndiyo makao makuu ya uovu wote unaoendelea duniani leo. Baada ya mambo yote, yaani mwisho wa nyakati, kuzimu na kila kilichomo ndani yake vitatupwa kwenye ziwa la moto wa milele.
✍Wanadamu wanaokufa ndani ya Yesu wako paradise sasa hivi. Baada ya mwisho wa mambo yote, wataingia Yerusalemu mpya na kuishi pamoja na Bwana milele na milele.
*Usipange kukosa kuingia Yerusalemu Mpya!*
0767103520
Mathiaselias27@gmail.Com

Maoni
Chapisha Maoni