ZITAFAKARI NJIA ZAKO

*πŸ–Š ZITAFAKARI NJIA ZAKO πŸ–Š*

24 January 2019

Morning glory

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

SAUTI YA MUNGU MINISTRY πŸ’’


Bwana Yesu Kristo apewe sifa


πŸ–Š Rafiki yangu katika Yesu Kristo nimeona kicheko hapa dunia siku hizi napenda nikuambie pia ujue.

πŸ–Š Rafiki zama hizi ni za hatari mno naam ,ni za hatari sana maana wateule wengi wanapotezwa.


πŸ–Š Rafiki mbona unakimbilia kutabiriwa na watu wajiitao mitume na manabii❓

πŸ–Š Mbona wakimbilia sana mahubiri ya mafanikio ya mwilini na kuyaacha mahubiri ya kukulia wokovu yaani mahubiri yatakayookoa roho yako ❓

πŸ–Š Mbona watafta hayo huku hata kufanya kazi ni mzembe unahubiriwa utapata gari unaitikia Ameeen .Wewe ni mnafiki kwa sababu huwezi kupata gari huku hufanyi kazi kwa bidii .

πŸ–Š Tangu uwatafte wanaokuhubiria mafanikio hawahawahi kukwambia dhambi inaua usipotubu unatafta injili za kuzimu za watu wamejiingiza kwa kujitaftia fedha wameshindwa kufanya kazi wakabuni mbinu ya kukuchuna pesa hata kuanza kukuuzia mpaka keki ,mafuta ,chumvi na maji wanayaita ya upako ❌❌❌❌
Ni ubatili ni ubatili umemwacha kumtegemea Yesu Kristo wategemea vitu vya kiganga ole wako 😑😑

πŸ–Š Wapotezwa kwa mafundisho ya uongo hujiulizi tu na pia unatafta miujiza hujui kwamba kuna watumishi miujiza yao ni ya kishetani ❓Hawa Yesu Kristo hawajui na siku ya hukumu atawasukumia jehanamu .


πŸ“– 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 7 :21

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

Mathayo 7 :22

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Mathayo 7 :23

πŸ–Š Miujiza watatenda lakini siyo ya nguvu za Mungu Bali ni ya nguvu za mashetani huku wamevalia macheni na mapete makubwa yenye nguvu hizo .

πŸ–ŠUjitafakari usitafte kutabiriwa .

πŸ“– *Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.*


Mathayo 24:24

πŸ–Š Usitafte miujiza na ishara na ajabu za uongo mpaka zinawekewa matangazo ni ubatili ❌❌❌

πŸ–Š  Wengi wamewekewa mikono na watumishi hawa wamepokea roho za mashetani .


Zitafakari njia zako

Mungu akubariki


Kupata masomo haya kila siku pakua app yetu

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*