HUTATUKANWA TENA πŸ–Š*

*πŸ–Š HUTATUKANWA TENA πŸ–Š*




Night service

27 February 2019

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



πŸ“– *30 Nami nitazidisha matunda ya miti, na mazao ya mashamba, msipate tena kutukanwa na mataifa kwa sababu ya njaa.*


Ezekieli 36 :30



πŸ–Š Shetani anatumia kigezo cha umaskini kuwatukana wana wa Mungu .


πŸ–Š Wengi amewadanganya na kuwa awape utajiri ili wawe na maisha ya fraha na ya kushiba wakamtumikia wakaangamia .


πŸ–Š Wengine wameona mali wakaolewa wakitazamia wataishi maisha yasiyo na njaa kushiba wameshiba lakini amani ndani ya ndoa haipo.


πŸ–Š Ni heri kuvumilia njaa ya mda mfupi ikiwa ni mapenzi ya Mungu umsuburi akuinue ili usitukanwe na mataifa kuliko kukimbilia shibe mikononi mwa shetani ukapata aibu ya milele .


πŸ–Š Naam , shetani ni muongo sana angalia hapa uongo aliotaka kumwingizia Yesu Kristo

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ“– 5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.

Luka 4 :5

6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

Luka 4 :6

7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.

Luka 4 :7

8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

Luka 4 :8

πŸ–Š Alipomwangalia Yesu Kristo alifikiri anashida na vitu anavyomwonyesha kumbe .


πŸ–Š Vivyo hivyo na leo shetani asije akakukuta katika hali ya chini akatumia njia hiyo kukucheka akisema njoo kwangu unitumikie.Hii mabinti wachunge sana wanakosea wenzi kwa kuangalia vitu kuliko tabia za mume .



πŸ‘•sitamani vitu heri uchekwe huna kuliko kufuata vitu ukamezwa na ibilisi


πŸ–Š Tambua wakati unakuja aliyekucheka atashuhudia umeinuliwa sana.



Mungu akubariki sana

Simama katika imani

πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻πŸ’ͺ🏻

Pakua app yetu kupata masomo mengine

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*