KUMWOMBEA MGONJWA

πŸ’’ SOMO: *NAMNA YA KUMWOMBEA MGONJWA* πŸ’’



Mwl .PETER FRANCIS MASANJA

0679392829

SAUTI YA MUNGU MINISTRY

Pakua app yetu kupata masomo mengine

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry





TUOMBE

Baba katika jina la Yesu ni wewe ndiye ujazaye mioyo yetu furaha ,amani , upendo, na kutupa sisi afya na uzima , achilia nguvu ya roho wako kwa anayesoma ujumbe huu ukamfundishe kuvunja vifungo vya magonjwa ambavyo watu wako wamefungwa na mfalme wa giza yaani shetani na malaika zake ( wachawi na waganga , mapepo na majini ) katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth , fungua moyo wa msomaji wa ujumbe huu apate kuelewa ujumbe huu na apate maarifa ya kushindana na kushinda kwelikweli kupitia jina la Yesu .Amen
 

1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Mathayo 10 :1

πŸ‘‰BWANA YESU ASIFIWE .

Leo nimepata kibali cha kukushirikisha kwenye hili somo ili ujifunze na kuongeza maarifa zaidi ya kiroho na uzidi kustawi na kuishi maisha ya ushindi katika ulimwengu wa roho na unaoonekana .

✝ Nikukumbushe tu kwamba

1. siyo kila ugonjwa unaougua ni mpango wa Mungu

2. Siyo kila ajali ni mpango wa Mungu

Katika ulimwengu wa roho , shetani huwatumia mawakala wake kukutengenezea ajali na magonjwa ambayo hupelekea kifo .

πŸ‘‰Katika jina la YESU roho ya ajali toka , roho ya magonjwa sugu na yaliyokosa vipimo toweka , achia maisha ya msomaji wa ujumbe huu ,toweka katika jina lipitalo majina yote la BWANA wetu YESU KRISTO wa Nazareth. Amen

πŸ’’ FUATA HATUA HIZI KUMFUNGUA / KUMWOMBEA MGONJWA

πŸ”₯ SAMBARATISHA VIKAO WALIVYOKAA KUMUUA HUYO MGONJWA

Wachawi na waganga hukaa kikao kwanza kabla ya kumuua mtu .

15 Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.
Isaya 54 :15

20 Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo;
Matendo ya Mitume

 1 :20

Kiri Maombi haya
Baba katika jina la Yesu , ninasambaratisha vikao vya waganga na wachawi waliopanga kumuua huyu mgonjwa ( kama unamjua jina mtaje ) ikiwa ni kwenye anga , ardhi.  na bahari .Amen

πŸ”₯ SHUGHULIKIA MALANGO YA MAUTI NA KUZIMU YANAYOTAKA KUMWUA HUYO MGONJWA

πŸ‘‰ Mtu auguapo malango ya mauti na kuzimu hukaa kwake ,ndyo maana wagonjwa waliozidiwa huwaza kufa tu kwa sababu rohoni mwake anaona mauti inamwandama.

13 Wewe, Bwana, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,

Zaburi 9 :13

18 Nafsi zao zachukia kila namna ya chakula, Wameyakaribia malango ya mauti.

Zaburi 107 :18

17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?
Ayubu 38 :17

πŸ‘‰Yafunge malango ya mauti na kuzimu yaliyomkamata huyo mgonjwa .

πŸ”₯ ISEMESHE ROHO YA MAUTI IACHIE UHAI ,NAFSI NA ROHO YA HUYO MGONJWA

Mauti ni roho inayosikia nguvu za giza .Mauti husafiri na inatumwa ikiambatanishwa na jina la mtu .

Isemeshe roho ya mauti itoke kwa mgonjwa

14 Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.

Hosea 13 :14

Sema:Ee roho ya mauti , mauti ya kifafa,maumivu ya mgongo, kiuno , miguu ,mikono, magonjwa ya mapafu, tumbo, figo, moyo n.k mwachie huyu mgonjwa , katika jina la Yesu. Amen

πŸ”₯ FUTA HABARI AU HATI YA KIFO ALIYOANDIKIWA HUYO MGONJWA

πŸ‘‰ Katika ulimwengu wa roho , wachawi na waganga wanapokaa kikao cha kutakumuua mtu wanapanga yafuatayo :

1.Aina ya kifo ( ugonjwa au ajali)

2. Mahali( sehemu /eneo ) ambapo mtu atafia

3. Siku
 atakayokufa

4. SAA ya kufa huyo MGONJWA(mtu )

5. Tarehe ya kifo

14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Wakolosai 2 :14

πŸ”₯OMBA ULINZI KWA AJILI YA HUYO MGONJWA

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;

Isaya 62 :6

MUNGU AKUBARIKI πŸ’’


YEREMIA 51:20_23

20 Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;
Yeremia 51 :20

21 na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;
Yeremia 51 :21

22 na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke;
Yeremia 51 :22

23 na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.
Yeremia 51 :23


πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’πŸ’’

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*