MPANGO WA BWANA KUHUSU MAWAZO YETU

MPANGO WA BWANA KUHUSU MAWAZO YETU.


 *SEHEMU YA KWANZA*  

         0767103520

✍Mawazo yetu ni muhimu sana kwa maisha yetu ya sasa na yale yajayo. Kwa hiyo, Mungu anayo mengi ya kusema kuyahusu. Ametuwekea utaratibu na mwongozo wa kuweza kuvuna baraka zake kwa kupitia kwenye mawazo yetu. Hata hivyo ni muhimu kukumbuka wakati wote kuwa

*Msaada wetu unatoka kwa Bwana.* (Zaburi 124:8).

Pia Yeye anasema: *Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.* (Yohana 15:5).


Kwa hiyo, hata katika suala la kuwaza au kutafakari, bila msaada wake, hatuwezi kitu. Kama kuwaza tu kwa namna inayofaa hatuwezi, sembuse kuyafanya hayo mawazo yetu yatupatie shauku za mioyo yetu? Agizo la muhimu analotupa Bwana, tunalopaswa kulizingatia ni kuwa, *Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe.* (Mithali 3:5).


Bwana anasema nisizitumainie akili zangu!

Hili ni jambo la kushangaza kabisa. Kuzitumainia akili maana yake ni kufanya mambo yangu bila kumpa Mungu nafasi. Yaani, nikishawaza jambo tu, ninalitenda.

Tena ninakuwa ninajua tu kuwa yale yote ninayoyafanya ni ujanja, uwezo na juhudi zangu mwenyewe.


✍Mungu anatuonya kuhusu kuzitumainia akili, si kuhusukuzitumia. Tunatumia akili zetu kuchagua wapi pa kutumainia. Biblia inasema, *Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi.*(1Wakorintho 15:34)


*JINSI YA KUWA NA MAWAZO YENYE NGUVU*

✍Hivi itakuwaje kama nitaweza, kila siku, kuwa na mawazo ya kushinda, kuweza, kufanikiwa, kupona na mengine ya namna hii hata kama kwa namna ya kibinadamu mambo yanaonekana kuwa ni mabaya?

Bila shaka maisha yangu yatabadilika kwa haraka sana kuelekea kwenye ubora. Tunaweza kabisa kuzifunza akili zetu kuwaza mawazo chanya na si mawazo hasi, yaani tunaweza kuwa na imani. Na uzuri ni kwamba yupo Bwana upande wetu ambaye anatusaidia katika kila hatua.


*Kutofautisha nia*

✍Ili tuweze kujenga tabia ya kutafakari kwa mafanikio, ni lazima tuwe na uwezo wa kuchunguza na kutambua nia iliyomo ndani mwetu kila wakati.


✍Ndani mwetu kuna nia za aina mbili. Biblia inasema, *Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.* (Warumi 8:6).

Kwa hiyo, kuna nia ya mwili na nia ya roho.

Nia ya mwili ni nia ambayo hujificha sana kiasi kwamba wakati mwingine ni vigumu kuigundua.

Bila shaka umeshawahi kukutana na hali zifuatazoπŸ‘‡πŸ‘‡


πŸ”–Unapotaka kulala unaomba ulinzi wa Mungu uzingire nyumba yako. Lakini, baadaye ukisikia kishindo chochote nje, unaingiwa na hofu kubwa.

πŸ“Kilichokufanya uombe ni nia ya roho, lakini kilicholeta hofu ni nia ya mwili. Hii imekufanya usimwamini Mungu ambaye hapo tu kabla uliomba ulinzi wake.

πŸ”–Unaposafiri, unalifunika gari kwa damu ya Yesu. Lakini, gari likiyumba kidogo tu njiani, hukumbuki tena maombi uliyofanya. Hofu inaletwa na nia ya mwili.

πŸ”–Unaweza kuomba Bwana akufungulie milango ya mafanikio, kisha baada ya muda mfupi unaanza kusema hali ni ngumu, maisha ni magumu. Nia ya roho ilikusukuma kuomba lakini nia ya mwili ikakufanya ukiri kutowezekana.

πŸ”–Watumishi wa Mungu wanaposema kuwa Bwana ametupa mamlaka ya kutoa pepo na kuponya wagonjwa, unashangilia na kupiga makofi. Lakini ukiangalia, hujawahi kumwombea mgonjwa yoyote wala kukemea pepo. Nia ya roho ilikufanya upige makofi ya furaha lakini nia ya mwili inakuzuia kuyatendea kazi mambo hayo.


πŸ“’Mifano hii michache inatuonyesha kuwa, kumbe kwa nje unaweza kuonyesha kuwa uko upande wa Mungu, lakini ndani yako ukawa uko kinyume kabisa. Shida ni kwamba, ile nia ya ndani ambayo iko kinyume na Mungu ndiyo inakuwa na nguvu, na ndiyo inayoshinda. Kibaya zaidi ni kuwa, unakuwa hujitambui kwamba una hali hiyo.

Mathiaselias27@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*