MPANGO WA BWANA KUHUSU MAWAZO YETU
MPANGO WA BWANA KUHUSU MAWAZO YETU
*SEHEMU YA PILI*
0767103520
*Kuchagua nia sahihi*
✍Ili upate mazao mengi na bora shambani ni lazima ufanye kazi. Lakini, ili upate magugu mengi na mazao yako yaharibiwe, unatakiwa ukae tu bila kufanya chochote. Magugu yatakuja yenyewe tu. Hayahitaji juhudi yoyote. Akili ya mwanadamu ni kama shamba. Mawazo safi ni mazao bora. Mawazo mabaya ni magugu. Usipojibidisha kwa lolote kuhusu mawazo yako, ni lazima utavamiwa na lundo la magugu, yaani mawazo yasiyofaa! Wakati mwingine unaweza usilitambue hilo.
✍Dalili zinazoonyesha kuwa akili yako ina magugu hayo ni hizi zifuatazo: kusonya kila mara, kunung’unika, kulaumu watu wengine, kukosa raha, kujiinamia, kutikisa kichwa, kushika tama, kukosa usingizi, n.k.
✍Ili uwe na mawazo bora yatakayozaa matunda mema maishani, ni lazima ufanye kazi ya kung’oa magugu wewe mwenyewe, kwa maana, *Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu.* (Mithali 16:1).
✍Ni lazima kufanya uchaguzi wa makusudi (conscious selection) wa mawazo mema kutoka katika Neno la Mungu, na kuyatafakari hayo muda wote. Kufanya uchaguzi wa makusudi maana yake ni kuwa, usiache tu mawazo yoyote yaingie na kutoka akilini kama yapendavyo. Simama katika mlango wa akili yako kukagua kila wazo linalojitokeza, kisha ruhusu yaingie yaliyo safi na zuia yaliyo magugu.
πNi lazima kuitambua nia ya mwili kila wakati na kuishinda kabisa na kubaki na nia moja tu – ya roho. Unaishinda kwa kukiri neno la Mungu. Kwa mfano, unapoingiwa na hofu, unasema, *Imeandikwa kuwa Mungu hajanipa roho ya woga bali ya nguvu.*
✍Kitendo cha wewe kusema hivyo kinadhihirisha kuwa umetambua kwamba kuna magugu, yaani nia isiyo sahihi. Kwa njia hiyo tu ndipo utaona nguvu za Mungu zikifanya kazi maishani mwako. Hili ni jambo la muhimu sana! Endapo hufanyi hivyo, uwezekano mkubwa ni kuwa uko katika kundi la wale ambao hawajui kuwa
wamevamiwa na wanaendeshwa na hiyo nia ya mwili.
✍Kumbuka kuwa, mwanzoni hii itakuwa ni vita kubwa. Utapata upinzani mkubwa. Hili ni jambo la kawaida kabisa. Maana kuhusu adui zetu, Bwana anasema, *Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja nchi isiwe ukiwa na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.* (Kutoka 23:29-30).
✍Kasi ya kushinda kwako inategemea kuongezeka kwako - katika ufahamu, maarifa na nguvu. Kwa hiyo, Bwana anatutia moyo akisema, *Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.* (Yoshua 1:9).
✍Ukidumu katika kuyazuia mawazo mabaya kuingia akilini mwako kwa kutafakari mawazo mema kutoka katika neno la Mungu, hakika yake, baada ya muda mfupi utaona unabadilika kabisa! Hakika! Kwa maana, *neno hilo ni roho na roho ndiyo itiayo uzima!* (Yohana 6:63).
πKwa mfano, unapoumwa, badala ya kutafakari jinsi mwili unavyouma na udhaifu ulio nao, tafakari kwamba, *Kwa kupigwa kwake mimi nimepona; yeye ameyachukua magonjwa yangu. Mimi ni mzima katika Jina la Yesu.*
πUnapoishiwa fedha, badala ya kutafakari jinsi ambavyo shida uliyonayo ni kubwa kuliko fedha unayopata, tafakari, kwa mfano, *Yote yawezekana kwa imani. Kwa Jina la Yesu naamuru fedha zije kwa ajili ya hitaji hili nililonalo.*
✍Kwa kufanya hivi, utakuwa unatimiza andiko linalosema, *Linda sana moyo wako maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.* (Mithali 4:23). Uzima haushii kwenye kupona tu magonjwa. Hata kupata fedha, chakula na nguo ni sehemu ya uzima. Ndani ya moyo kuna chemchemi itakayotoa huo uponyaji na hizo fedha ambayo ni mahitaji yako.
✍Ukiyawaza yale yaliyo kinyume na neno la Mungu, unakuwa katika kundi hili: *Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.* (Mithali 25:25). Utaanza tu kukiri udhaifu na kushindwa. Hatimaye, utavamiwa na roho za kuzimu za kila namna, maana hauna ulinzi. Na hizo ndizo zitakazokudidimiza chini zaidi na zaidi ili litimie andiko lisemalo, *Mauti …. huwa katika uwezo wa ulimi.* (Mithali 18:21).
*Chagua mawazo ya kutafakari! Usikubali hata kidogo kuwa mtumwa wa mawazo. Usitawaliwe na mawazo, bali uwe mtawala wa mawazo. Yaani, wewe Ndiyo uchague nini cha kuwaza na nini cha kutupa nje.Kisha utaona ahadi za Mungu zikitimia maishani mwako*
Mathiaselias27@gmail.com

Maoni
Chapisha Maoni