KUWA RAFIKI WA MUNGU

*πŸ–Š MUNGU ANATENDA KAZI NA MARAFIKI ZAKE πŸ–Š*

Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829

πŸ–Š Rafiki wa Mungu ni yule atendaye ambayo Mungu kamwaamuru kutenda.

πŸ–Š Rafiki wa Mungu ni yule aliyejitoa kwaajili ya kumtumikia Mungu na kuishi maisha matakatifu .

πŸ“– *Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo* .

Yohana 15:14

πŸ–Š Kuongea na Mungu ni jambo jepesi ukiwa mtii .

πŸ“– *Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake.* Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumishi wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana, hakutoka mle hemani.

Kutoka 33:11

πŸ–ŠMtu akiwa rafiki wa Mungu atapata mengi toka kwake .

πŸ–Š Kwa kawaida marafiki hufanana tabia na mwenendo

πŸ–Š Mungu ni mtakatifu na rafiki zake pia ni watakatifu ndio anatembea nao pamoja .

πŸ“– *Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu*

Mambo ya Walawi 11:45

πŸ–Š Ukitaka kupishana na Mungu kuwa rafiki wa dunia

πŸ“– *Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.*

Yakobo 4:4

πŸ–Š Unapoipenda dunia na starehe zake umekuwa adui wa Mungu na hivyo Mungu hawezi kukubariki .

πŸ–ŠTengeneza urafiki na Mungu ili ajishughulishe na mambo yako .

πŸ–Š Au ni nani amwonaye rafiki yake ampendaye yupo na shida asimsaidie ❓

πŸ–Š Vivyo hivyo Mungu ukiwa rafiki yake atakusaidia hatakuacha kamwe.

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

πŸ”° MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA πŸ›*