MSINGI WA MAOMBI

*🖊 UOMBAPO OMBA KWAAJILI YA KUMFANYIA MUNGU JAMBO 🖊*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829


📖 20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Mwanzo 28 :20

21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.
Mwanzo 28 :21

22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Mwanzo 28 :22


🖊 Kile alichokiomba Yakobo alikiomba ili akitumie kwa ajili ya kazi ya Mungu .

🖊 Hakuomba ili ashindane na watu au ajionyeshe kwa watu .Aliomba ili kubarikiwa kwake kuambatane na kufanya kazi ya Mungu .



📖 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.

Yakobo 4:3



🖊 Aliomba ili atumie kwa kazi ya Mungu na siyo kwa tamaa zake .

🖊 Nakukumbusha uombapo zingatia utamfanyia nini Mungu ?

🖊 Maana wengi akiwabariki humsahau na kugeukia dunia .


📖 12 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;
Kumbukumbu la Torati 8 :12

13 na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;
Kumbukumbu la Torati 8 :13

14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau Bwana, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
Kumbukumbu la Torati 8 :14

15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,
Kumbukumbu la Torati 8 :15

16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
Kumbukumbu la Torati 8 :16

17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
Kumbukumbu la Torati 8 :17

18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kumbukumbu la Torati 8 :18


🖊 Kama kwa biashara ndogo tu umemsahau je akikupa kubwa utamkumbuka kweli ?

🖊 Katika kazi zako mtukuze Mungu .





Mungu akubariki sana

Pakua app yetu kwa masomo ya kila siku


https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*