NAKUANDIKIA HAYA UYAFAHAMU

*🖊 NAKUANDIKIA HAYA UYAFAHAMU 🖊*


Mwl.Peter Francis Masanja

0679392829



🖊 Matendo mema hayampeleki mtu mbinguni ❌❌


🖊 Jifikirie sana , unaweza ukatenda mema kwa watu na ukawa mwovu kabisa mbele za Mungu .


🖊 Fikiria hata kahaba na mwizi anaweza kutendea watu mema .


🖊 Fikiria wengine ni wafanya kazi wanaiba fedha na huku pia wanasaidia watu .


🖊 Fikiria wazinzi nao hujitoa kuhudumia familia za watu na kusomesha mabinti za watu 😁😁😁


🖊 Njia nzuri ya kuurithi uzima wa milele ni kuwa mtakatifu mbele zake Mungu bila kusahau kumkiri Kristo .



🖊 Tenda mema kwa watu huku ukiishi dhambini ukifa watasema ulitenda mema , hayo mema Mungu hayajui kama hukuwa Mtakatifu

Watasema R.I.P bure haikufanyi Mungu akupe kibali cha kuingia katika ufalme wa mbinguni .


Uwe makini sana siyo kila atendaye mema ataingia katika ufalme wa mbinguni
Bali yule aishie maisha matakatifu

Rejea Mathayo 7:21-23


Tambua basi kuwa si kila atendaye mema kwa watu ataurithi ufalme wa mbingini bali yule mtakatifu .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*