NGUVU YA MSAMAHA
NGUVU YA MSAMAHA
Mwl Peter Francis Masanja
0744056901
Msamaha
ni nini ?
Kabla
ya kujua maana ya msamaha tuelewe kwanza maana ya neno kusamehe.
Kusamehe
ni kuahirisha au kuondoa hasira, chuki, na kinyongo juu ya mtu aliyekukwaza au
kukuumiza nafsi yako.
Sasa
tunaweza kuangalia maana ya msamaha
Msamaha
ni kitendo cha kuondoa uchungu au manung'uniko juu ya mtu aliyekukosea.
ASILI YA MSAMAHA NI
WAPI
Au
Je , msamaha chanzo chake ni wapi
Huwezi kusamehe kama hujui mwanzilishi wa
msamaha ni nani .
Mwanzilishi
wa msamaha ni Mungu kupitia amri iitwayo Upendo .
Asili ya msamaha ni upendo , bila upendo mtu
hawezi kusamehe.
Msamaha
hapa duniani uliletwa na Mungu kwa njia ya Upendo .
16
Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana
3:16
Mungu
alipomtoa Kristo afe kwaajili ya dhambi zetu sababu kuu ilikuwa ni sisi
kusamehewa .
Lakini
kabla ya neno kusamehewa kitu kikuu kilikuwa ni kwamba alitupenda na anatupenda
mpaka sasa .
Kwahiyo
, Msamaha asili yake ni ndani ya sheria au amri ya Mungu iitwayo Upendo .
Upendo
ni amri kuu ya Mungu ambayo ndani yake imebeba amani , furaha, na msamaha (
kusamehe).
13
Basi,
sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni
upendo.
1
Wakorintho 13:13
Mungu
alitoa amri hata juu ya wanandoa , alitanguliza neno kupenda ndiyo akaamuru
kusameheana kila mmoja .
Ukimpenda mtu hutakuwa na uchungu naye .
19
Ninyi
waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
Wakolosai
3:19
Ukiona
mume anakwaruzana na mke wake utambue kuwa mume amevunja amri iitwayo upendo .
Pasipo
upendo hakuna msamaha wala amani .
13
mkawastahi
sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
1
Wathesalonike 5:13
✍🏻
Kwahiyo , asili ya Upendo yatoka kwa Mungu na ndani ya upendo kuna msamaha.
Upendo
ni shina la msamaha.Shina hili likiondolewa msamaha hautapatikana.
✍🏻
Amani huletwa kwa kanuni kuu mbili .
1
Upendo
2.
msamaha
8
Yeye
asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
1
Yohana 4:8
16
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni
upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani
yake.
1
Yohana 4:16
Mtu
wa Mungu tulikuwa tunaangalia asili ya msamaha na chanzo chake , twende
kipengele kifuatacho ✍🏻✍🏻
FAIDA YA MSAMAHA( KUSAMEHE
) KIROHO
Mtu
wa Mungu kuna faida kubwa sana ya kusamehe kiroho .
Ø Msamaha Unamfanya Mungu Akusamehe
Dhambi .
Utusamehe
deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo
6:12
Mtu
wa Mungu , kama unaikiri sala ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake na kuna
mtu hujamsamehe ujue wamdhihaki Mungu .
Unapoukiri
huu mstari katika sala hii inamaana kwamba umeshasamehe adui zako ( waliokukosea
).
Kama
ukikiri hujasamehe na Mungu hawezi kukusamehe makosa yako .
Ndyo
maana unaweza ukajikuta unajisikia uchovu ndani ya ibada kumbe hujasamehe na
Roho wa Mungu amekuacha hunafraha na ibada .
15
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa
yenu.
Mathayo
6:15
Msamaha
ni amri ya Mungu ambayo imo ndani ya amri iitwayo upendo .
Ukiivunja
hii amri maana yake bado watembea gizani yaani hujasamehewa dhambi zako .
Ø Msamaha Unamfanya Mungu Aikubali
Sadaka Yako Na Maombi Yako .
23
Basi
ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno
juu yako,
Mathayo
5:23
24
iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako,
kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo
5:24
Sadaka
yako inaweza ikakataliwa na Mungu endapo hutasamehe .
Hata
kama utamtolea wingi wa sadaka gani kama hujasamehe sadaka yako itaitwa ni
sadaka ya mwenye dhambi .
11
Huu
wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta
ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu
ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.
Isaya
1:11
12
Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu,
kuzikanyaga nyua zangu?
Isaya
1:12
Unaweza ukawa mtoaji mzuri sana kwa Mungu
lakini kutokusamehe kukakufanya mambo yako yawe mabaya.
Maana
yake ni kwamba kwa njia ya kusamehe tunasamehewa makosa yetu na tukisamehewa
makosa yetu sadaka zetu hukubaliwa na
BWANA .
Unatakiwa
ujue kwamba sadaka yako inapokubalika mbele za Mungu hufungua mlango wa baraka
kwako wewe na uzao wako .
25
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na
Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko
11:25
26
Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi
makosa yenu.]
Marko
11:26
Mungu anapoiangalia sadaka yako uitoayo wakati
hujasamehe waliokukosea huona mbele yake kasimama muuaji kutoa sadaka .
Maana yake huwezi ukaitenga chuki na kumwazia
mtu mabaya , maana yake ukiwa umemchukia mtu ujue kabisa wewe ni muuaji na
uuaji ni dhambi .
21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue,
na mtu akiua, itampasa hukumu.
Mathayo
5:21
22
Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu
akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya
moto.
Mathayo
5:22
Jitathmini ni wapi uliapa hutasamehe , kisha futa hivyo
viapo maana vitakutia jehanamu .
v msamaha
unatoa kibali mbele za Mungu .
Kibali maana yake ni kukubalika mbele za Mungu
na kupewa nguvu za kumiliki na kutawala .
Mtu mwenye kusamehe hatatumia nguvu nyingi
sana kwenye maombi , atapeleka hoja zake kwa Mungu naye atamjibu haraka.
Unaweza ukawa unajifikiria swali hili
Kwanini tangu nioe uchumi wangu unazidi kuwa
mbaya ❓ yaani kila ukijaribu mradi unakufa .
Jibu
ni kwamba
Ø Mungu
kakunyima kibali cha kutawala na kumiliki kwa sababu hutaki kumsamehe mke wako
kila siku mnagombana .
kila
siku umemnunia mkeo na humuiti tena mke wako
Eti
ukitaka kumwita unasema
Wewe
,au fulani njoo
7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama
chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima,
kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe .
1
Petro 3:7
Kumbe unaweza ukakwama kiroho na kusema una
mikosi kwasababu hujamsamehe mke wako .
Jitathmini inawezekana hali mbaya ya uchumi
wako ni kwasababu hupo vizuri na mwenzi wako .
Ndoa iliyobarikiwa ni ile ambayo wakipishana
husameheana na kusahau hii inakibali .
Mungu akubariki sana
Karibu
tena siku nyingine tuendelee
Nakukaribisha
kwa maswali
Ubarikiwe sana kwa somo zuri binafsi limenibariki sana na kunifanya kuwa mwepesi wa kusamehe lakini nimejifunza kuwa bila upendo huwezi kusamehe
JibuFuta