NGUVU YA MSAMAHA


                  NGUVU YA MSAMAHA

Mwl Peter Francis Masanja
0744056901

Msamaha ni nini ?
Kabla ya kujua maana ya msamaha tuelewe kwanza maana ya neno kusamehe.
Kusamehe ni kuahirisha au kuondoa hasira, chuki, na kinyongo juu ya mtu aliyekukwaza au kukuumiza nafsi yako.
Sasa tunaweza kuangalia maana ya msamaha
Msamaha ni kitendo cha kuondoa uchungu au manung'uniko juu ya mtu aliyekukosea.

                        ASILI YA MSAMAHA NI WAPI

Au Je , msamaha chanzo chake ni wapi
 Huwezi kusamehe kama hujui mwanzilishi wa msamaha ni nani .
Mwanzilishi wa msamaha ni Mungu kupitia amri iitwayo Upendo .
 Asili ya msamaha ni upendo , bila upendo mtu hawezi kusamehe.
Msamaha hapa duniani uliletwa na Mungu kwa njia ya Upendo .
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3:16
Mungu alipomtoa Kristo afe kwaajili ya dhambi zetu sababu kuu ilikuwa ni sisi kusamehewa .
Lakini kabla ya neno kusamehewa kitu kikuu kilikuwa ni kwamba alitupenda na anatupenda mpaka sasa .
Kwahiyo , Msamaha asili yake ni ndani ya sheria au amri ya Mungu iitwayo Upendo .
Upendo ni amri kuu ya Mungu ambayo ndani yake imebeba amani , furaha, na msamaha ( kusamehe).
13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
1 Wakorintho 13:13
Mungu alitoa amri hata juu ya wanandoa , alitanguliza neno kupenda ndiyo akaamuru kusameheana kila mmoja .
 Ukimpenda mtu hutakuwa na uchungu naye .
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
Wakolosai 3:19
Ukiona mume anakwaruzana na mke wake utambue kuwa mume amevunja amri iitwayo upendo .
Pasipo upendo hakuna msamaha wala amani .
13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
1 Wathesalonike 5:13
🏻 Kwahiyo , asili ya Upendo yatoka kwa Mungu na ndani ya upendo kuna msamaha.
Upendo ni shina la msamaha.Shina hili likiondolewa msamaha hautapatikana.
🏻 Amani huletwa kwa kanuni kuu mbili .


1 Upendo

2. msamaha

8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
1 Yohana 4:8
16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.
1 Yohana 4:16
Mtu wa Mungu tulikuwa tunaangalia asili ya msamaha na chanzo chake , twende kipengele kifuatacho 🏻🏻
                                                                
                    FAIDA YA MSAMAHA( KUSAMEHE ) KIROHO

Mtu wa Mungu kuna faida kubwa sana ya kusamehe kiroho .
Ø  Msamaha Unamfanya Mungu Akusamehe Dhambi .
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

Mathayo 6:12
Mtu wa Mungu , kama unaikiri sala ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake na kuna mtu hujamsamehe ujue wamdhihaki Mungu .
Unapoukiri huu mstari katika sala hii inamaana kwamba umeshasamehe adui zako ( waliokukosea ).
Kama ukikiri hujasamehe na Mungu hawezi kukusamehe makosa yako .
Ndyo maana unaweza ukajikuta unajisikia uchovu ndani ya ibada kumbe hujasamehe na Roho wa Mungu amekuacha hunafraha na ibada .
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Mathayo 6:15
Msamaha ni amri ya Mungu ambayo imo ndani ya amri iitwayo upendo .

Ukiivunja hii amri maana yake bado watembea gizani yaani hujasamehewa dhambi zako .
Ø  Msamaha Unamfanya Mungu Aikubali Sadaka Yako Na Maombi Yako .

23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

Mathayo 5:23
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
Mathayo 5:24
Sadaka yako inaweza ikakataliwa na Mungu endapo hutasamehe .
Hata kama utamtolea wingi wa sadaka gani kama hujasamehe sadaka yako itaitwa ni sadaka ya mwenye dhambi .
11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema Bwana. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo waume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi waume.
Isaya 1:11

12 Mjapo ili kuonekana mbele zangu, ni nani aliyetaka neno hili mikononi mwenu, kuzikanyaga nyua zangu?
Isaya 1:12                

  Unaweza ukawa mtoaji mzuri sana kwa Mungu lakini kutokusamehe kukakufanya mambo yako yawe mabaya.
Maana yake ni kwamba kwa njia ya kusamehe tunasamehewa makosa yetu na tukisamehewa makosa yetu sadaka zetu hukubaliwa na  BWANA .
Unatakiwa ujue kwamba sadaka yako inapokubalika mbele za Mungu hufungua mlango wa baraka kwako wewe na uzao wako .
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11:25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]


Marko 11:26
 Mungu anapoiangalia sadaka yako uitoayo wakati hujasamehe waliokukosea huona mbele yake kasimama muuaji kutoa sadaka .
 Maana yake huwezi ukaitenga chuki na kumwazia mtu mabaya , maana yake ukiwa umemchukia mtu ujue kabisa wewe ni muuaji na uuaji ni dhambi .
 21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
Mathayo 5:21
22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Mathayo 5:22
Jitathmini  ni wapi uliapa hutasamehe , kisha futa hivyo viapo maana vitakutia jehanamu .
v  msamaha unatoa kibali mbele za Mungu .

 Kibali maana yake ni kukubalika mbele za Mungu na kupewa nguvu za kumiliki na kutawala .
 Mtu mwenye kusamehe hatatumia nguvu nyingi sana kwenye maombi , atapeleka hoja zake kwa Mungu naye atamjibu haraka.
 Unaweza ukawa unajifikiria swali hili
 Kwanini tangu nioe uchumi wangu unazidi kuwa mbaya ❓ yaani kila ukijaribu mradi unakufa .
Jibu ni kwamba
Ø  Mungu kakunyima kibali cha kutawala na kumiliki kwa sababu hutaki kumsamehe mke wako kila siku mnagombana .
kila siku umemnunia mkeo na humuiti tena mke wako
Eti ukitaka kumwita unasema
Wewe ,au fulani njoo
7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima,
 kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe .
1 Petro 3:7

 Kumbe unaweza ukakwama kiroho na kusema una mikosi kwasababu hujamsamehe mke wako .


 Jitathmini inawezekana hali mbaya ya uchumi wako ni kwasababu hupo vizuri na mwenzi wako .
 Ndoa iliyobarikiwa ni ile ambayo wakipishana husameheana na kusahau hii inakibali .
 Mungu akubariki sana

Karibu tena siku nyingine tuendelee
Nakukaribisha kwa maswali


Maoni

  1. Ubarikiwe sana kwa somo zuri binafsi limenibariki sana na kunifanya kuwa mwepesi wa kusamehe lakini nimejifunza kuwa bila upendo huwezi kusamehe

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA YA KUJAA ROHO MTAKATIFU

NGUVU NA FAIDA ZA MSAMAHA

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*