Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2018

🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐*

Picha
🔰 MBINU ZA KUFUNGA NA KUOMBA 🛐* Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 🔰 BWANA YESU ASIFIWE 🖊 Nakukaribisha tena katika somo hili wewe ndugu au rafiki yangu wa imani tujifunze kwa pamoja . 🖊 Kufunga na kuomba kuna faida kubwa sana kwa kila aliyempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake 🛐 *NAMNA GANI UTAFUNGA NA KUOMBA* ? 🖊 Utakapoanza kufunga na kuomba utaona mafanikio makubwa sana kiroho .Sasa unatakiwa upitie hatua fulani ili upate muda mzuri wa kuzungumza na Mungu . 🛐 *HATUA ZA KUFUATA KATIKA KUFUNGA NA KUOMBA* 🔰 1⃣ _WEKA MALENGO YAKO📖🖊 🔰 Kwanini unafunga ? Je unafunga kwa sababu ipi ama kwa 👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻 🖊 Kurudisha uhusiano wako na Mungu 🖊 Kutafta uongozi wa Mungu 🖊 Kutafta uponyaji . 🖊 Kwa ajili ya suluhu ya tatizo 🖊 Kutafta namna ya kutatua tatizo . Mwambie Roho Mtakatifu akuongoze na kukupa maelekezo katika malengo ya kufunga kwako . Hii itakusaidia uombe kwa kulenga kwenye eneo maalumu na kwa...

NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA💪🏻*

Picha
 *🔰 NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA💪🏻* SIKU YA PILI  Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 📖 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe. Ezekieli 2:1 🖊 Maranyingi ni vigumu sana kupokea majibu ya matatizo yako kama utategemea mtu asimame aseme na Mungu kwaajili yako . 🖊 Baada ya kifo cha Yesu Kristo pale msalabani ,Mungu alimimina Roho Mtakatifu kwa kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake . 🖊 Kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake amepewa mamlaka ya kiroho endapo atasimama imara katika maombi akilitumia jina la Yesu Kristo wa Nazareti . 🖊 Katika somo lililopita tuliona maana ya jina la Yesu Kristo na uweza lililobeba ndani yake. 🖊 Leo tuangalie mamlaka iliyobebwa na hili jina la Yesu . 1⃣ MAMLAKA JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA NA NGUVU ...

NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA

Picha
 💪🏻 NAMNA YA KUJISIMAMIA MWENYEWE KATIKA MAOMBI UKITUMIA MAMLAKA ILIYOMO NDANI YA JINA NA DAMU YA YESU KUUSHINDA UFALME WA GIZA SIKU YA KWANZA Mwl Peter Francis Masanja  0679392829  UTANGULIZI ✍🏻 Katika somo hili kila aliyempokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake aweze kujisimamia mwenyewe akitumia jina na damu ya Yesu Kristo kushinda nguvu na ufalme wa giza ✍🏻 Kuna wakati mtu anatafta msaada wa kuombewa ombewa halafu yeye haombi anasubiri aombewe na kumwuliza mwombaji majibu ya maisha yake. ✍🏻 Hii ni mbaya sana kushindwa kujisimamia mwenyewe katika maombi ✍🏻 Nataka nikwambie kwamba ukimpokea Yesu Kristo kama Bwana na mwokozi wa maisha yako umetangaza vita na shetani ✍🏻 Kwahiyo ili shetani asikunase na mitego yake lazima uvae silaha kuu zifuatazo. 1⃣ Neno  2⃣ Jina na damu ya Yesu 3⃣ Utakatifu  4⃣ Bidii,katika,maombi ✍🏻 ,Haya ni mambo unatakiwa kuyazingatia sana baada ya kumpokea Yesu ✍🏻 ...

JIWEKE TAYARI

Picha
🖊 *JIWEKE TAYARI* 🖊 Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 💻 _40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu. Luka 12 :40 Bwana Yesu Kristo apewe sifa Neno la Mungu linatukumbusha kwa habari ya kujiweka tayari mimi na wewe . 🖊 Ni vema tutambue kwamba kujiweka kwetu tayari hakupo kufanya maandalizi ya kimwili . 🖊 Hapa tunatahadharishwa kwa habari ya kudumu sana katika utakatifu maana hatujui siku wala saa ajapo Yesu Kristo kuwahukumu walio hai na wafu . 🔰 Kuna wakati tunatakiwa kujua kwamba ujio wa Yesu ni sawa na kifo mtu hawezi kujua kufa kwake ni mda gani yaani ni saa ngapi atakufa . Apataye ajali na kufa papo hapo alikuwa hajui kama atakufa kwa ajali . 🖊 Mungu anatutaka tufanye maandalizi maana hata kufa kwetu hatujui . 🖊 Sasa kama kesho yetu ni fumbo je tukifa tukiwa hatujatubu mwisho wetu ni upi❓ 🔰 Nataka nikwambie wewe rafiki yangu na ndugu yangu katika Yesu Kristo kwamba usiishi na dhambi unajua ni dham...

MOYO WA MWANADAMU

Moyo wa mwanadamu ni kama shamba ambalo inawezekana hilo shamba lina vichaka au magugu au mawe au visiki n.k Lakini shamba hilo likisafishwa huwa shamba safi. Hata shamba lolote lazima liwe linasafishwa kila baada ya muda ndipo litabaki kuwa shamba safi. Na moyo wa mwanadamu nao kama shamba unahitaji kusafishwa ili uwe safi. Kuna njia njia mbili za kusafisha moyo yaani kutubu na kuacha dhambi. Maombi ya toba husafisha moyo ili yasiyotakiwa moyoni yatoke. Moyo kama shamba hauhitaji kusafishwa Mara moja tu Bali usafi unatakiwa uwe wa kila Mara ndipo moyo kama shamba utapaki safi siku zote. Hakikisha katika maisha yako unahusika sana na maombi ya kutubu kisha jitenge siku zote na maovu. Zaburi 51:1-2 " Ee MUNGU, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu." Ukipanda mbegu katika shamba chafu ujue mbegu hiyo haitaota au itaota lakini haitastawi. Toba katika KRISTO YESU ni...