Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2018

KUHUSU MARAFIKI

*PUNGUZA MZIGO, PUNGUZA MARAFIKI FEKI PUNGUZA KABISA TENA WAPUNGUZE SANA TU;WAPUNGUZE ILI UWE MWEPESI* *Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao wako right kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea. Punguzaaaa!* *Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi. Punguzaaaa!* *PU

MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUFANYA MAAMUZI YA KUOA AU KUOLEWA

❓ MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUFANYA MAAMUZI YA KUOA AU KUOLEWA 🍇 Je , unaye mtu mwingine aliyeingia kwa njia ya uzinzi ❓ Kama unaye mng'oe kwanza anaweza kuwa kizuizi kwako kumpata mwenzi sahihi . 🍇 Umeamua kweli kuoa au kuolewa ❓ ✍ Usiolewe kwa sababu umechoka kukaa nyumbani au umri unaenda . 🍇 Utaolewa lini na nani utampa mwili wako ❓ ✍ Tambua kuwa mwili wako ni wa mume wako peke yake tu . ✍ Na wewe kijana unaoa lini , nani unamuoa❓ 🍇Utaoa au utaolewa wapi na kivipi ❓ ✍ Usikubali kuolewa kienyeji 🍇Unajua kuwa ndoa itakubadilishia mfumo wa maisha yako ❓ ✍ Utaacha wazazi , utahama maeneo ya kazi , utaacha baadhi ya marafiki , utakuwa Mrs fulani au Mr fulani . 🍇 Unajua kuwa ndoa ni wajibu ❓ ✍ Ndoa siyo starehe tu kijana . Na Mwl.Peter Francis Masanja

LAZIMA UJUE TOFAUTI KATI MTU NA MWANADAMU

  🍇 LAZIMA UJUE TOFAUTI KATI MTU NA MWANADAMU 🍇 Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 ✍ Mtu anatabia ya kimungu ndani yake .Amebeba utu ( matendo ya haki ). ✍ Mwanadamu amebeba tabia za mnyama ( anatenda mambo kama mnyama ) .Kila kitu kwake kufanya ni sawa tu .   ✍ Mwanadamu anaroho ya uasi ndani yake na anafanya uadui na Mungu . 📖 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mwanzo 1:26 ✍ Mtu anasura na mfano wa Mungu yaani utendaji wake ndani yake . ✍ Mwanadamu yeye anaunyama ndani yake Akijisikia aoe wake wengi anaoa , akijisikia akalewe au akanunue makahaba anaenda tu kwasababu anasifa kama mnyama .   📖 1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, Mwanzo 6:1 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wo

MAOMBI YA TOBA JUU YA URITHI MBAYA

           MAOMBI YA TOBA JUU YA URITHI MBAYA SEHEMU YA KWANZA Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 0744056901 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, Kutoka 20:5 Bwana Yesu asifiwe. Karibu sana katika mwongozo wa maombi haya ambayo nimeyaandaa ili yaweze kukusaidia katika maisha yako na rafiki zako pia . Roho wa Mungu amenigusa kuandika haya maombi ili yaweze kukufungua pale unapoona kuna shida lakini umeshindwa kujua namna ya kuingia katika toba. Katika maombi haya nataka nikupe onyo kwanza kwamba maana ya toba ni kukubali kuachana kabisa ulichokuwa unakitenda na kuamua kukaa karibu na Mungu muumba mbingu na nchi,aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Nakusihi sana na narudia kukusisitiza kwamba unapotubu hakikisha hurudii tena hiyo dhambi. Maishani mwako kuna mambo mengi sana ambayo yanamchukiza Mungu na

📖 JINA ULILOPEWA LINA MAANA GANI KIROHO ❓

                📖 JINA ULILOPEWA LINA MAANA GANI KIROHO ❓ Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 📖 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. Yohana 17:12 ✍ Yesu alipewa jina kubwa sana kiroho na jina lenye nguvu za kuokoa litajwapo mashetani hutetemeka. ✍ Jina la Yesu lina mamlaka na nguvu za kushinda ufalme wa giza. 📖 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Yohana 17:11   Jina ulilopewa yaani jina la ukoo lina maana gani ❓ ✍ Kuna majina ya ukoo yanaambatana na miungu ya ukoo ✍ Jina ulilopewa nyumbani yaani jina la asili linaweza likawa limebeba tabia mbaya na roho za miungu zitakazo sumbua maisha yako. ✍ Jina la ukoo lina tabia , fuatilia kujua tabia zake, ✍ Unaweza kupewa jina la babu yako aliyekuwa m

OKOKA KATIKA MAMBO YOTE

                  📖OKOKA KATIKA MAMBO YOTE 📖 Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 Kuokoka ni kukataa ubaya . Kuokoka ni kukataa uvionavyo vizuri lakini ni machukizo kwa Mungu. Kuokoka ni kuishi maisha matakatifu. Kuokoka ni kuishi kama Kristo alivyoishi . Kuokoka ni kusoma neno na kulifanyia kazi na kuliishi. Kuokoka ni kutubu na kuacha dhambi usirudie tena . Kuokoka ni kufunga na kuomba .Kama hufungi na kuomba bado hujaokoka . Kuokoka ni kuachana na marafiki waovu na kutafta marafiki watakao kufanya ukue kiroho. Kuokoka ni kuacha kuabudu miungu na kuamua kumwabudu Mungu aliye hai , Muumba mbingu na nchi . Kuokoka ni kumpenda Mungu 📖 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 1 Yohana 2:15 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 1 Yohana 2:16 ✍ Kinywa chako kiokoke . Epuka matukano

BE CLOSE TO GOD

 BE CLOSE TO GOD  Teacher: Peter Francis Masanja 0679392829 Praise the Lord,     YOU WILL NOT BE LOST BECAUSE OF THE FOLLOWING THINGS: ·          Fornication ·          Adultery ·          Anger ·          Anxiety ·          Enemies ·          Bad friends ·          Jokes ·          Temptations ·          Psychological torture ·          Diseases ·          Hunger ·          Poverty God will make your life good and keep you away from your   enemies and every situation that makes you feel bad.Be closer to him .   'It is good for me to be near you. I choose you as my protector, and I will tell about your wonderful deeds. Powerful LORD God, all who stay far from you will be lost, and you will destroy those who are unfaithful. ' Psalms 73:27-28 Ø   Our God ,Almighty says that , he will save you when you walk in his ways . Ø   You will be given power and strength by your Lord. Ø   God will never leave you forever. Ø   It is this