FAIDA YA KUFUFUKA KWA YESU
🌐 FAIDA YA KUFA NA KUFUFUKA KWA YESU KATIKA MAISHA YAKO 🌐 Mwlm.Peter Francis Masanja The voice of God Ministry 0679392829 💫Bwana Yesu asifiwe 💻 51 Na tazama , pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini ; nchi ikatetemeka ; miamba ikapasuka ; Mathayo 27 :51 52 makaburi yakafunuka ; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala ; Mathayo 27 :52 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake , wakauingia mji mtakatifu , wakawatokea wengi . Mathayo 27 :53 ✍🏻Leo napenda nikushirikishe ili tuweze kuangalia faida za kifo cha Yesu pale msalabani pamoja na kufufuka kwake . 💻 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3 :16 💫Kwanza tutazame lengo kuu la Yesu kuletwa duniani ambalo kila mtu amwaminiye apate uzima wa milele . 💫Il...