Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2019

UASHERATI USITAJWE KWAKO

*πŸ–ŠUASHERATI USITAJWE KWAKO πŸ–Š* 1 February 2019 Morning glory Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 πŸ“– Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; Waefeso 5:3 πŸ–Š Kijana yeyote aliyeokoka asipatikane na uasherati . πŸ–Š Kijana yeyote aliyeokoka asiuchafue mwili wake kwa uasherati πŸ–Š Bali asubiri aoe au aolewe kama iwastahilivyo watakatifu. πŸ–Š Naam , Uasherati ni kitendo cha kujihusisha na michezo ya ngono kabla ya ndoa ( sex before marriage ). πŸ–Š Kwa kijana aliyeokoka huu ni uchafu na unamuua kiroho na kimwili . πŸ–Š Naam , hii huja kusumbua ndoa sana . Kwa mapana zaidi tembelea somo langu liitwalo Kwanini ujitunze mpaka uoe au uolewe ❓ https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sauti.ya.mungu.ministry

SOMO KUHUSU KUZIMU

SOMO KUHUSU KUZIMU *SEHEMU YA TATU* Kwa nini inaitwa mauti ya pili? Ni kwa sababu japo tajiri yuko kwenye mateso na hayuko duniani tena (yaani alishakufa); japo wale malaika walio kifungoni wako kwenye mateso sasa; lakini iko mauti nyingine tofauti nay a sasa. Kitendo cha kutupwa kwenye ziwa la moto (jehanamu) na kubaki humo milele ndicho kinachoitwa mauti ya pili. ✍Hata roho hii ya mauti inayotutoa duniani sasa pamoja na kuzimu aliko shetani sasa navyo vitaingia jehanamu kwenye mauti ya pili: Imeandikwa: *Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. (Ufu 20:14)* *JE, ROHO ZILIZOONDOKA DUNIANI ZINAKUWA KATIKA HALI GANI?* Hawa ni watu kamili kama tulivyo sisi. Sisi kama roho tumo ndani ya mwili wa nyama, lakini ukivua mwili huu (yaani, ukifa) unavikwa mwili wa kiroho; na unaendelea kuishi kama kawaida. Biblia inasema: *Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, n

SOMO KUHUSU KUZIMU

SOMO KUHUSU KUZIMU *SEHEMU YA PILI* Bwana alipokuja duniani, akateswa na akauawa, tunaambiwa kuwa: *Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri. (1Petro 3:18-19)* ✍Mbinguni hakuna vifungo; vifungo viko chini ya nchi. Kwa hiyo, Bwana alienda kuwahubiria waliokuwa kifungoni. ✍Bila shaka hii ndiyo sehemu ambayo Wakatoliki huita toharani. Sehemu hii ilikuwapo zamani kama makao ya muda kwa wale waliokufa kabla ya Kristo. Humo waliwekwa kungojea ukombozi wa mwanadamu ufanye na Kristo. Lakini sasa hivi haipo tena. ✍Maana ya andiko hili katika Petro ni kuwa, wale waliokuwa kifuani mwa Ibrahimu (au tuseme toharani), Bwana alienda akawahubiria katika zile siku tatu alipokuwa katika tumbo la nchi. *Je, baada ya kuwahubiria, nini kilifuata?* Imeandikwa: *Hivyo husema, alipopaa juu alit

SOMO KUHUSU KUZIMU

SOMO KUHUSU KUZIMU  *SEHEMU YA KWANZA* WATU WAKIFA, ROHO ZAO ZINAKUWA WAPI? Biblia inasema kuhusu Bwana Yesu kuwa:πŸ‘‡πŸ‘‡ Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; (Wafilipi 2:9-10). ✍Kulingana na mstari huu, tunagundua kuwa kuna sehemu kuu tatu:                                                  Mbinguni                                                  Duniani                                                  Chini ya nchi ✍Mbinguni ni mahali aliko Mungu; duniani ni mahali tuliko sisi wanadamu tulio hai; na chini ya nchi ni mahali aliko ibilisi. ✍Tangu nyakati za Adamu kulikuwapo wanadamu wema na waovu. Wanadamu wema walikufa na waovu nao walikufa. Swali ni kuwa, je, walipokufa walienda wapi? Mwinjilisti Luka anatupatia picha nzuri kutokana na kisa alichosimulia Bwana Yesu juu ya tajiri na Lazaro. Tunasoma katika Luke 16:22-26

KIBALI NA WITO

*πŸ–Š KIBALI NA WITO* πŸ–Š Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 SAUTI YA MUNGU MINISTRY πŸ–Š Bwana Yesu Kristo apewe sifa . πŸ–Š Leo tuangazie tofauti kati ya kibali na wito . πŸ“– 7 *Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.* Mwanzo 4 :7 πŸ–Š Tunamwona Kaini hakubarikiwa na Mungu kwa sababu hakutenda vema yaani sadaka aliyoitoa haikuwa njema kwa Mungu . πŸ–Š Kibali ni majibu ya chanya ya kile ukiombacho mbele za Mungu . πŸ–Š Kibali ni baraka ambayo mtu anaipata kutoka kwa Mungu.. πŸ–Š Kibali ni matokeo mazuri ya kitu ambacho mtu kakiomba kuonyesha kuwa maombi yake yamekubaliwa . πŸ–Š Kaini hakupata majibu ya maombi yake kwa sababu sadaka yake haikumpendeza Mungu . πŸ–Š Vivyo hivyo hata leo watu hawapati majibu ya maombi yao yaani kibali kwasababu ya dhambi au kutokujua kuomba . πŸ–Š WITO Wito au kuitwa na Mungu ni kitendo cha Mungu kumweka mtu kwaajili ya kutimiza kusudi au kufan

ZITAFAKARI NJIA ZAKO

*πŸ–Š ZITAFAKARI NJIA ZAKO πŸ–Š* 24 January 2019 Morning glory Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 SAUTI YA MUNGU MINISTRY πŸ’’ Bwana Yesu Kristo apewe sifa πŸ–Š Rafiki yangu katika Yesu Kristo nimeona kicheko hapa dunia siku hizi napenda nikuambie pia ujue. πŸ–Š Rafiki zama hizi ni za hatari mno naam ,ni za hatari sana maana wateule wengi wanapotezwa. πŸ–Š Rafiki mbona unakimbilia kutabiriwa na watu wajiitao mitume na manabii❓ πŸ–Š Mbona wakimbilia sana mahubiri ya mafanikio ya mwilini na kuyaacha mahubiri ya kukulia wokovu yaani mahubiri yatakayookoa roho yako ❓ πŸ–Š Mbona watafta hayo huku hata kufanya kazi ni mzembe unahubiriwa utapata gari unaitikia Ameeen .Wewe ni mnafiki kwa sababu huwezi kupata gari huku hufanyi kazi kwa bidii . πŸ–Š Tangu uwatafte wanaokuhubiria mafanikio hawahawahi kukwambia dhambi inaua usipotubu unatafta injili za kuzimu za watu wamejiingiza kwa kujitaftia fedha wameshindwa kufanya kazi wakabuni mbinu ya kukuchuna pesa hata kuanza kukuuzia mpaka k

ZITAFAKARI NJIA ZAKO

*πŸ–ŠZITAFAKARI NJIA ZAKO* πŸ–Š Morning glory 23 January 2019 Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 SAUTI YA MUNGU MINISTRY πŸ–Š Bwana Yesu Kristo apewe sifa πŸ–Š Nikukumbushe tu kuwa Musa aliambiwa avue viatu vyake maana mahali alipokuwa amekanyaga ni patakatifu yaani ni pasafi hapanuki dhambi yoyote. πŸ–Š Hii ni kwa sababu aliyekuwepo pale kwenye kijiti naye ni mtakatifu , kwahiyo ilimbidi Musa naye avue uchafu ili aweze kumsogelea . πŸ–Š Inawezekana kabisa rafiki yangu unamwomba Mungu akutendee jambo fulani lakini huoni matokeo . πŸ–Š Inawezekana tatizo ni njia zako mbaya yaani matendo yako maovu hayo ni kiatu kinakuzuia Mungu kumfanya awe rafiki yako I'll uombapo asikie kuomba kwako . πŸ–Š Dhambi hiyo ni kiatu kinakuzuia kumkaribia Mungu na kumfanya asizungumze na wewe . πŸ–Š Kivue hicho kiatu yaani dhambi kwa kutubu na kuacha kabisa ili Mungu azungumze na wewe kama Musa alivyoweza kuvua viatu vyake πŸ“– 5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako;

HUDUMA NI NINI*

Picha
πŸ–Š * HUDUMA NI NINI* ❓ Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 Huduma ni kazi ambayo mtu kapewa na Mungu aifanye kwa uongozi wa Roho Mtakatifu  kwaajili ya kuwafanya watu wamjue Mungu na kudumu katika maisha matakatifu ili wawe na uzima wa milele . πŸ–Š Huduma ni kazi apewayo mtu na Roho wa Mungu ili apeleke ujumbe wa Mungu kwa watu . πŸ–Š Mfano 1⃣ Utume 2⃣ Unabii 3⃣ Uchungaji 4⃣ Uinjilisti 5⃣ Ualimu πŸ“– 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 1 Wakorintho 12 :5 28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, *wa kwanza mitume* , wa *pili manabii* , *wa tatu waalimu,* kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha. 1 Wakorintho 12 :28 29 Je! *Wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu?* Wote wanatenda miujiza? 1 Wakorintho 12 :29 πŸ–Š Huduma ni kazi ya Kiroho πŸ“– Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; W

ZITAFAKARI NJIA ZAKO

πŸ–Š ZITAFAKARI NJIA ZAKO πŸ–Š 17 January 2019 Morning glory Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 πŸ–Š Wewe baba, mama, kaka na dada . πŸ–Š Ujana ni kipindi ambacho mwili unashindana na roho ❓ πŸ–Š Ujana ni kipindi cha vita vikali sana dhidi ya dhambi na lazima uishinde dhambi πŸ–ŠLakini nina neno juu yako nalo ni hili πŸ–Š Katika maisha yako usiishi maisha ya dhambi ukisema utatubu tu ipo siku . πŸ–Š Au kijana mwenzangu unajua siku na saa yako ya kufa ❓ πŸ–Š Ujue kufa siyo mpaka uumwe unaweza kudondoka tu ukafa au ukalala usiku ndyo kufa kwako huamki tena ⚰ πŸ–Š Unakumbatia dhambi gani unajifariji utatubu tu ❓ πŸ–Š Jiulize ikitokea saivi umekata roho utaenda mbinguni siku ya hukumu au utaenda jehanamu ❓ πŸ–Š Basi acha njia mbaya jiweke tayari maana hujui ni saa ipi na mda gani Yesu Kristo anakuja Vivyo hivyo na kufa kwako hujui ni lini . Somaaa hapaa✍🏻✍🏻✍🏻✍🏻 πŸ“– 40 Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu. Luka 12 :40 πŸ–Š

SILAHA ZA KIROHO

✍🏻 SILAHA ZA KIROHO πŸ–Š πŸ“–SOMO LA KWANZA πŸ“– Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 πŸ“– 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Waefeso 6 :11 πŸ–Š Bwana Yesu Kristo asifiwe πŸ–Š Tukivitafakari vita vya rohoni tunaona kuna falme mbili yaani ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani . πŸ–Š Lakini ufalme wa Mungu ni mkuu na unanguvu kuliko ufalme wa shetani . πŸ–Š Pia tunaona kuwa kuna mamlaka mbili za kiroho πŸ–ŠMamlaka ( Authority ) ni nguvu ya kuamua/kuamuru jambo litokee au lifanyike . πŸ–Š Zitazame hizi mamlaka 1⃣ Mamlaka ya Mungu . πŸ–Š Mamlaka hii ni kuu kuliko mamlaka zote .Hakuna mamlaka iwezayo kuishinda mamlaka ya Mungu . 2⃣ Mamlaka ya shetani πŸ–Š Hii ni mamlaka itendayo kazi hapa duniani kwa lengo la kuiba , kuua na kuangamiza .Mamlaka hii imejaa uongo na na ni dhaifu hainauwezo wa kuishinda mamlaka ya Mungu . πŸ–ŠPia kuna wakuu wawili naam 1⃣ Mungu ni mkuu sana πŸ–Š Mungu ni mkuu kwa watu wake na huwapa watu kushinda na amewapa w

OMBEA FIKIRA

*πŸ–Š TAMBUA UMUHIMU WA KUOMBEA FIKIRA ,MAWAZO NA AKILI YAKO πŸ–Š* Somo la 1 Mwl.Peter Francis Masanja 0679392829 πŸ“– 1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12 :1 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; *bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,* mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12 :2 πŸ“– Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. Msiige mitindo ya ulimwengu huu, *bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu.* Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu. Waroma 12:1‭-‬2 BHND πŸ“– And so, dear brothers and sisters, I plead with you to give your bodies to