KUUSAFISHA MOYO
📒 KUUSAFISHA MOYO 📙* 💻 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11 💫 Moyo hauwezi ukaliweka neno kama haujausafisha vizuri 💻 Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki. Hosea 10:12 💫 Neno la Mungu haliwezi kukaa moyoni mwako likastawi kama kuna magugu yanayozuia lisiote . 💫 Moyo ni shamba la kiroho Sasa kama kuna magugu udogo hautakuwa mzuri kwa mbegu kuifanya mizizi ipate nafasi ya kuufanya mmea ukue vizuri . 💫 Twende tuyaone haya magugu yanayozuia neno la Mungu lisikae moyoni mwa mtu . 💻 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; Mathayo 15:19 💫 Magugu yanayozuia neno la Mungu lisizae matunda moyoni mwa mtu ni 📙 MAWAZO MABAYA 📙 UUAJI 📙UZINZI 📙 UASHERATI 📙 WIVI 📙 USHUHUDA WA UONGO 📙 MATUKANO ...