MAFUNDISHO YA AWALI BAADA YA MTU KUOKOKA.
MAFUNDISHO YA AWALI BAADA YA MTU KUOKOKA. Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU. Leo nina somo fupi kuhusu watu waliookoka karibuni au watu waliookoka zamani ila hawajui wafanyeje. Kuna watu waliwahi kuniomba niandae somo kuhusu mafundisho ya awali baada ya mtu kuokoka. Hii ni sehemu tu ya Masomo kuhusu kipengele hicho. Hata mimi Katika utumishi wangu kwa KRISTO YESU Mwokozi wangu kuna watu kadhaa niliwaongoza sala ya toba, na wengine walinipigia simu ili niwaongoze sala ya toba maana ndio walikuwa wameamua kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wao. Nilifanya hivyo na MUNGU akajitwalia utukufu. Hakika YESU KRISTO anaokoa wote wanaoamua kumpokea na kumtii kupitia Neno lake, Bwana YESU anasema ''Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. - Yohana 10:28'' Mimi nilipompokea Bwana YESU ilikuwa ni Mwishoni mwa mwaka 2008, Baada tu ya kuokoka nilianza juhudi ya...